Ukipewa Talaka Unatakiwa Kulipwa 50% ya Mali

Wanandoa wametakiwa kuishi kwa kuheshimu na kufuata matakwa ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inayowataka wanandoa kuheshimu viapo vyao, ambayo imeainisha mume au mke ana haki ya kudai fidia pindi unapopewa talaka.

Akizungumza na eatv.tv mwanasheria na wakili wa kujitegemea Addo Mwasongwe amesema kuwa ni halali kisheria mwanandoa kudai fidia ya mali asilimia 50 kwa 50 kama wamechuma pamoja mali hiyo.

“Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 sura ya 29, iliyorekebishwa mwaka 2002 kifungu cha 9 inaeleza ndoa za aina zote kuwa zimesajiliwa na kuwa na vitambulisho ili kuwepo uhalali wa ndoa hiyo na inampa mwanandoa ambaye aliingia kwenye ndoa na kuanza kuchuma mali na mwenzake anaruhusu kudai sehemu ya mali anaopopewa talaka", amesema Addo .

Aidha ameongeza kuwa sheria ina walinda pia wasio wanandoa, endapo watathibitika kuishi pamoja kwa muda wa miaka miwili bila kufunga ndoa, sheria inawatambua kama mke na mume.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad