Ukweli kuhusu Mo Salah kuivaa Uruguay leo..Jibu Kama Atacheza Lipo Hapa

Kocha mkuu wa Misri Hector Cuper amesema mshambuliaji wa timu hiyo Mohamed Salah yupo kamili kwa asilimia takribani 100 kucheza mechi yao ya kwanza kweney fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay leo.


"Ninaweza kusema karibu asilimia 100 mchezaji Mo Salah yuko vizuri kucheza mchezo wa wetu dhidi ya Uruguay, yeye binafsi yupo tayari kucheza tunachojaribu sisi ni kumpa ujasiri tu'', amesema Cuper.

Mohemed Salah aliumia bega kwenye mchezo wa fainali ya UEFA Mei 26, kufuatia kukumbana na mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos. Awali ilihofiwa kuwa huenda akakosa fainali hizo lakini sasa inaonekana yupo vizuri kuiwakilishi nchi yake.

Misri ambayo ipo Kundi A na timu za Russia, Saudi Arabia na Uruguay leo itaanza rasmi kampeni ya kusaka ubingwa wa dunia ambapo haikupata nafasi ya kucheza fainali hizi tangu mwaka 1990 ambapo Salah alikuwa hajazaliwa.

Mechi hiyo itachezwa majira ya saa 9:00 Mchana kwa saa za Afrika Mashariki, kwenye uwanja wa Yekaterinburg. Uwanja huo una uwezo wa kuingiza mashabiki 35000 lakini utapunguzwa hadi 23000 baada ya fainali za Kombe la Dunia.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad