URUSINI: Mtanzania atakata kombe la dunia kule Urusi, ampiku Messi kwa Magoli


Wakati Sanchez na Icard wakiangalia mpira kwenye TV, fahamu kuna mtanzania anakichafua huko Urusi kama hana akili nzuri. Anaitwa Yussuf Yurary Poulsen aliyezaliwa 15 June 1994. Jana ilikuwa siku yake ya kuzaliwa. Huyu kijana ni mtanzania mwenzetu. Kwa bahati mbaya alichagua fungu lililojema zaidi kwake. Hivi maajuzi alimaliza kiu ya mabao kwa Wadenmark baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Mexico.



Hivi leo Poulsen amefunga bao la pekee kwenye mtanange wao dhidi ya Peru kwenye Kundi C. Hii ni mara baada ya Peru kukosa penati ya mwendokasi iliyopigwa na Christian Cueva, kama ile ya Ali Kiba (Natania).

Poulsen amewaadhibu waperu ipaswavyo kunako dakika ya 59. Poulsen alimwangusha Cueva kwenye eneo la hatari na mwamuzi Bakary Gassama alikwenda kujiridhisha kwenye VAR na kisha kuwazawadia Peru penati.


Kwa bahati nzuri Cueva ajulikane kama “Aladdin” aliamua kupeleka mpira ule mwezini kama mvumo wa radi.

Poulsen angekuwa anaitumikia timu ya taifaya Tanzania basi walio wengi wangemtukana na kumkebehi sana kwa kusababisha penati. Poulsen ametoa mwanga kwa wazawa wa Tanzania kwamba lolote lawezekana cha msingi kujituma tu.

Wakati Lionel Messi akiteseka kuibeba Argentina kwa Poulsen mbona ilikuwa kazi rahisi tu? Poulsen ameonesha njia kubwa kwa wachezaji wazawa kwamba kila kitu kinawezekana.

Ni Mtazania mwenzetu ingawa kidogo yeye ameishi kwa wenzetu lakini bado ana damu ya kitanzania na anapaswa kutumika kama kielelezo halisi cha ufanisi ambao unapaswa kuvumbuliwa na kizazi cha ndani.

Alizaliwa katika jiji la Copenhagen huko huko Denmark. Alizaliwa na mama Mdenmark na baba yake alikuwa mfanyakazi wa meli aliyekuwa akifanya kazi hizo katika safari zake za Afrika na Denmark. Baba yake alifariki kwa Kansa Poulsen akiwa na miaka 6 tu. Poulsen amewahi kuja Tanzania mara kadhaa kutembelea familia ya upande wa baba yake mzazi.


Taarifa za chini zinasema kuwa Poulsen alikuwa na matumaini ya kuchezea Tanzania lakini hakuwahi kupata mwaliko wa TFF. Taarifa hizo sio rasmi ni fununu tu.
Mara kadhaa ameonekana akiwa amevalia tisheti yenye bendera ya Tanzania


Aina yake ya uchezaji ni mshambuliaji wa kati ambaye anasifika kwa kasi naa nguvu. Amekuwa akitumia sanna nguvu kitu kinachomfanya mwalimu amwamini.

Ameweka rekodi ya mchezaji mwenye asili ya Tanzania kucheza fainali za kombe la dunia tena mbaya zaidi amefunga bao katika mchezo wa mapema akimwacha mbali Messi mwenye mabao 0 hadi sasa baada ya kila mmoja kucheza mechi moja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad