Mpambano wa Ufaransa dhidi ya Australia umekamilika kwa mabao mawili kwa moja. Mchezo huu ulikuwa mgumu sana kwa waaustralia kwani safu yao ya ushambuliaji ilishindwa kupiga shuti hata moja.
Kiungo hatari wa klabu ya Man United Paul Pogba amezima ndoto za Australia za kupata angalau alama moja. Pogba alifunga bao murua kabisa. Pogba alipiga mashuti mawili na yote yalilenga goli. Pogba ameondoka uwanjani akigusa mpira kwa mara 70 akizidiwa mara 8 tu na N’golo Kante. Pogba amepiga pasi moja muhimu na alikuwa na wastani wa pasi kwa asilimia 86.
Pogba alikuwa upande wa kushoto wa Kante na alikuwa akisaidiana na Mbappe. Upande wake ndio ulionekana kuwa na nguvu zaidi. Anthonio Griezman alitolewa na kuingia Oliver Giroud. Watu wengi watajiuliza kwanini. Griezmann alipoteza mipira mingi sana huku akiwa na wastani wa pasi 57 tu hivyo kuonekana kuigharimu timu zaidi.
Safu ya ulinzi ya Ufaransa ilikuwa imara zaidi kwani Varane na Umtiti walisimama imara.
Mapungufu kadhaa yalikuwepo hasa kwenye maamuzi. Baadhi ya wachezaji walikuwa wanafanya maamuzi yaisiyo ya kiukomavu kama vile Mbappe pamoja na Pavard.
Maamuzi ya mwalimu ya kumleta Fekir na Giroud yalikuwa sahihi lakini yalimuhitaji zaidi Anthonio Martial. Kwa asilimia 90 Oliver Giroud hakufanikiwa kupokea mipira ya krosi ambayo ingeonesha umuhimu wake uwanjani.
Australia ni kama wamekuja kusindikiza. Nabbout pamoja na Rogic na Cruize ni kama walikiwa wanarukaruka. Hatuwezi kuwalaumu sana licha ya kwamba pongezi nyingi zimuendee Mooy ambaye alijitahidi kupigana viatu vyema pamoja na akina Kante na Tolliso.
Taarifa za hapo awali zilisema kuwa Griezman alimtabiria Pogba kuwa ni mchezaji anayefaa kuwa nahodha wa timu yoyote duniani. Na leo Pogba amethibitsha hilo.