Ushauri: Tumeshazaa Watoto Wawili na Huyu Mzee, Nataka Kijana Mwenzangu Nile Maisha

Baada ya kusumbuana na huyu mzee kwa miaka kumi sasa na kuzaa nae watoto wawili, nafikiri ni muda sahihi wa mimi kupata raha.

Nina miaka 20 ya mwishoni, huyu baba ndiyo mwanaume wangu wa kwanza na simjui mwanaume mwingine zaidi yake.

Alinikuta mdogo sana ushawishi wake na tamaa za ndugu zangu ukaniponza nikawa nae mpaka sasa.Ana familia yake na watoto wakubwa tunaolingana umri.

Nimegundua sijaenjoy maisha wala ujana kabisa sina cha kuhadithia naenda disco nikiwa na wapambe wake, madereva wake mwisho saa 6 mpaka 8 ananipitia tunaenda kulala, kitandani mzuri(labda sababu sijajua wengine.Jamani eti mbaba wa miaka 60 na zaidi anaweza kuwa mzuri kitandani au najidanganya?

Nataka nianze kujua vijana wenzangu, kama pesa ninayo, magari na kila mwanangu ana nyumba yake ila namiss kula maisha jamani. Je nitakosea? Huyu mzee nataka kumuacha kama watoto nishampa aniache na mimi nile ujana wangu.

Nipeni ushauri wenu na huyu baba sijui nimtokaje, nikimbie nijifiche nisahau kila kitu kama miaka 2 hivi yakinishinda narudi kwake au?

By Zahra White/JF
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad