Ushuru Pombe za Nje JUU....Za Ndani Utabaki Palepale

Ili kutimiza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda, imependekezwa kutofanyika mabadiliko ya viwango maalum vya ushuru wa bidhaa zisizo za petroli zinazozalishwa hapa nchini na kuongeza viwango vya ushuru wa bidhaa zisizo za petroli zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.

Akiwasilisha bungeni jana  mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi 2018/19, Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango alisema mapendekezo hayo ni pamoja na ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji baridi utaendelea kutozwa kwa kiwango cha Sh.61 kwa lita.

Aidha amesema ushuru wa bidhaa kwenye maji ya kunywa yaliyosindikwa kwenye chupa yaliyoagizwa kutoka nje utaongezeka kutoka Sh.61 kwa lita hadi Sh.64.05 kwa lita, ikiwa ni ongezeko la Sh.3.05 kwa lita.

Kadhalika, ushuru wa bidhaa kwenye maji yanayozalishwa hapa nchini utaendelea kutozwa kwa kiwango cha sasa cha Sh.58 kwa lita.

Pia amesema ushuru wa bidhaa kwenye maji ya matunda(juisi) iliyotengenezwa kwa matunda yanayozalishwa hapa nchini hautaongezeka na utaendelea kutozwa kwa kiwango cha Sh.9 kwa lita.

Hata hivyo amesema ushuru wa bidhaa kwenye maji ya matunda iliyotengenezwa kwa matubda ambayo hayazalishwi hapa nchini utaongezeka kutoka Sh.221 hadi Sh.232 kwa lita, hivyo ongezeko ni Sh.11 kwa lita.

Akizungumzia bidhaa ya bia, Dk.Mpango alisema ushuru wa bidhaa hiyo inayotengenezwa kwa nafaka ya hapa nchini ambayo haijaoteshwa hautaongezeka na utaendelea kutozwa kwa kiwango cha Sh.450 kwa lita.

Pia kwa bia zinazoagizwa kutoka nje ya nchi utaongezeka kutoka Sh.765 kwa lita hadi Sh.803.25 kwa lita,ikiwa ni ongezeko la Sh.38.25 kwa lita.

Waziri huyo amesema ushuru wa bidhaa kwenye bia zisizo za kilevi ikijumuisha vinywaji vya kuongeza nguvu vinavyoagizwa nje ya nchi utaongezeka kutoka Sh.561 hadi Sh.589.05 kwa lita, kwa bidhaa hizo zitakazozalishwa nchini zitatozwa kiwango cha sasa Sh.561 kwa lita.

"Kuanzisha ushuru wa bidhaa wa Sh.200 kwa lita kwenye mvinyo uliotengenezwa kutokana na usindikaji wa matunda (kama ndizi, rozela, nyanya) yanayozalishwa hapa nchini tofauti na zabibu kwa kiwango kinachozidi asilimia 75, "alisema
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad