UTAFITI: Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Boston nchini Marekani imebanishwa kuwa unywaji wa chai vikombe 2 kwa siku humuongezea mwanamke uwezo wa kushika ujauzito
Utafiti huo uliwahusisha Wanawake 3,600 na kuonesha kuwa wale wanaokunywa vikombe 2 vya chai kwa siku, wana 27% ya kupata ujauzito ikilinganishwa na ambao hawanywi chai
Aidha, Wanawake wanaotumia vinywaji baridi vya aina mbili kwa siku, hupunguza uwezekano wao wa kushika ujauzito kwa 20%
Hata hivyo, Mtafiti mmoja ameeleza kuwa utafiti zaidi unahitajika ili kujua kama chai ya kijani ndiyo husaidia wanawake kupata ujauzito au ni ya aina gani