AFYA: Imethibitika kwamba kukaa muda mrefu kwenye magari, ofisini au kwenye viti kunasababisha matokeo hasi kwa afya ya binadamu
Kukaa muda mrefu pia kunahusishwa na kusababisha uzito uliopitiliza, magonjwa ya moyo, kisukari na magonjwa mengine yasiyoambukiza
Kupitia utafiti mpya uliotolewa hivi karibuni, hamasa inatolewa kwamba baadhi ya shughuli za mwili ikiwemo njia rahisi za kuimarisha misuli zinaweza kumsaidia mtu kukabiliana na athari za kiafya za kukaa muda mrefu
Katika utafiti huo wataalamu walichambua data za watu 400,000 wenye umri wa kati nchini Uingereza
Watafiti hao walifanya ulinganifu wa ripoti za watu waliofanya shughuli za mwili kama mazoezi na muda waliotumia kuangalia runinga au kompyuta
Kutokama na uchambuzi huo wa data Wamebaini kuwa watu ambao wana misuli dhaifu wana uwezekano wa asilimia 31 ya kufa mapema kama watatumia saa mbili mbele ya runinga, ukilinganisha na watu wenye misuli imara ambao wanatumia muda kama huo
Pia watu hao wana hatari kwa asilimia 21 kupata magonjwa ya moyo na 14% kupata kansa ukilinganisha na wale wenye misuli imara.