Waangalizi EU Kutoka Nchi 46 Waanza Kazi Zimbabwe


Waangalizi EU Kutoka Nchi 46 Waanza Kazi Zimbabwe
Serikali ya Zimbabwe imesema itaendelea  na uchaguzi wake wa kwanza tangu kuondoka madarakani kwa Robert Mugabe licha ya mlipuko wa bomu uliotokea mwishoni mwa wiki iliyopita.

Msemaji wa polisi nchini Zimbabwe, Charity Charamba amesema mlipuko huo ambao nusra umpate Rais Emmerson Mnangagwa alipokuwa kwenye mkutano wa kisiasa, umesababisha vifo vya watu wawili.

Waangalizi kutoka nchi 46 na mashirika 15 ya kikanda na kimataifa wataangalia jinsi uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Julai 30 utakavyoendeshwa.

Katika uchaguzi wa urais, Emmerson Mnangagwa wa chama tawala ZANU-PF ambaye ana umri wa miaka 75 atapambana na mgombea wa chama cha muda mrefu cha upinzani cha MDC, Nelson Chamisa ambaye ana umri wa miaka 40.

 Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa wagombea hao wawili hawajaachana mbali na kinyang'anyiro kitakuwa kikali.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad