Wafanyakazi wa Sahara Media Group walala nje kushinikiza madai ya mishahara yao
0
June 26, 2018
Wafanyakazi wa Sahara Media Group walala nje kushinikiza madai ya mishahara yao
Na James Timber, Mwanza
Wafanyakazi wa Sahara Media Group wamehamishia makazi yao katika ofisi za utawala za kampuni hiyo kwa lengo la kushinikiza kupewa mishahara wanayomdai Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Anthony Diallo.
Wakizungumza mapema hii leo katika ofisi hizo zilizopo Wilaya ya Ilemela jijini hapa wameiomba Serikali ya Rais Dk. John Magufuli kuingilia ili haki yao ipatikane.
Julius Mkombe maarufu 'Dj Simba' alisema walipewa barua za kuvunja mkataba ikiambatana na likizo ya lazima, ambapo walikaa siku 28 na baada kurudi kazini wakawa hawajaelewana kwa walikuwa wanaongea na Mdogo wa Mmiliki wa Kampuni, walipoenda kwa Mwenye Kampuni alitoa ahadi kuwa watalipwa pesa zao ndani ya mwezi wa nne kufikia April 30, mwaka huu watamaliziwa pesa zao zote.
Alisema baada ya kufika hiyo tarehe wakawa wanakimbiwa na watu walioambiwa watashughulikia suala lao huku wakimpigia bosi wao anawajibu majibu yasiyo ridhisha, jambo linalopelekea watumishi wengine kufariki kutokana na ugumu wa maisha.
Naye Loyce Lubango ameeleza kuwa amefanya kazi kwa takribani miaka mitatu katika king'amzi cha Continental na hajalipwa mshahara toka mwaka jana mwezi wa tisa.
"huyu Diallo amenikwaza nampigia simu ananijibu nimtafute mmiliki wa continental na siyo yeye na nikimpa taarifa nakuja ofisini ananikimbia anategemea tule wapi, wakati tunamuona ana hela, alisema Lubango.