Wakati Mwingine Unaweza Usielewe Azam Wanataka nini

Uongozi wa Azam FC umemrufisha Mudathir Yahya kutoka Singida United na kumuongeza mkata wa miaka miwili.

Jafar Idd amesema usajili wa wachezaji wote wa sasa pamoja na kocha Juma Mwambusi kuwa ni mapendekezo ya kocha mpya Hans van Pluijm.

Wakati mwingine Azam wanaweza kukuchanganya kwa namna wanavyoendesha mambo yao ya mpira kwa sababu msimu uliopita tulishuhudia waliamua kuachana na kundi kubwa la wachezaji wao wa kikosi cha kwanza.

Wachezaji takribani watano (Manula, Gadiel, Kapombe, Nyoni, Bocco) ambao walijiunga  Simba na Yanga. Lengo la kuwaruhusu wachezaji hao kuondoka lilikuwa ni kuwapa nafasi vijana na tukawaona Shabani Idd (japo alikaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha) na Yahya Zayd.

Azam ilisajili wachezaji wengi lakini haikueatumia ipasavyo wachezaji hao, Wazir Junior hakucheza karibu msimu mzima wa ligi, Mabaraka Yusuph alikumbwa na majeraha. Msimu huu ndio ingekuwa wakati wa kuwatumia wachezaji  ambao waliwasajili lakini hawakutumika msimu uliopita.

Yahya Zayd na Shabani Idd wamethibitisha kwamba wana uwezo pamoja na Paul Peter ambaye anaibukia halafu wana washambuliaji wawiliabao ukianalia takwimu zao nje ya Azam ni nzuri. Wazir Junior kama aliweza kufunga magoli sita kwenye timu inayoshuka daraja uwezekano wa yeye kufunga mara mbili au mara tatu ya magoli aliyofunga akiwa Toto Africans ni mkubwa akiwa Azam.

Msimu huu plan yao ni ipi baada ya kuwasajili Tafadzwa Kutinyu, Donald Ngoma na Ditram Nchimbi ambao wote ni watu wazima babda kwa kuwa usajili wao ni wa kocha mpya Hans van Pluijm akisaidiwa na Mwambusi kwa hiyo kuna uwezekano wachezaji wanaosajiliwa sasa ndio watakaotumika sana msimu ujao.

Nafasi ya kina Shabani Idd na Yahya Zayd kupambana na kina Donald Ngoma na Kutinyu ipo wapi pamoja na hawa wengine akina Mbaraka Yusuph na Wazir Junior kwa sababu Azam kwa sasa ina rundo la washambuliaji.

Kwa kuwashauri Azam au wachezaji binafsi ni kwamba Wazir Junior, Mbaraka Yusuph, Paul Peter na Salmin Hoza watafutiwe timu wakacheze kwa mkopo kwa sababu huenda nafasi yao ikawa finyu msimu ujao.

Kukaa benchi hakuwezi kumsaidia mchezaji kuwa bora ndio maana Azam wameshawishika  kumrudisha Mudathir kwa sababu alikwenda Singida akacheza na kuonesha uwezo.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad