Walichoamua Jumuiya ya Waislamu juu ya wimbo wa Falz “This is Nigeria”


Siku kadhaa zilizopita staa wa muziki kutokea Nigeria Falz the bad guy alipewa siku saba kufuta video ya ngoma yake ya “This is Nigeria” kwenye mtandao wa Youtube na jumuiya ya kutetea haki za Waislamu nchini Nigeria MURIC.

Jumuiya hiyo ya MURIC imetangaza kuwa haitakwenda tena mahakamani kuishtaki video hiyo ikiwa Mkurungezi wa MURIC Prof Ishaq Akintola alisema kuwa “Hii italeta mchango chanya kwenye tasnia ya burudani, kukaa na kutunga sheria kali za kinidhamu kwa tasnia ya muziki na filamu kwa ujumla”

Falz alionekana kuomba radhi mbele ya Taasisi hiyo kutokana na kitendo cha kuwatumia wasichana waliovaa hijab katika kipande cha video ya wimbo wake “This is Nigeria” na jumuiya hiyo kuchukua maamuzi ya kumripoti na kumtaka aombe radhi na kuifuta video hiyo.

Kutokana na maamuzi ya Prof Ishaq Akintola alionekana kukubali msamaha wa Falz na kusema kuwa “Japo aliomba msamaha kidogo kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni, pia amejaribu kufafanua kuwa hakudhamiria kuwadhihaki Waislamu lengo lake lilikuwa ni kupiga kelele juu ya wasichana wa Chibok ambapo sisi tunafikiri ujumbe wake aliuwasilisha kwenye njia isiyo sahihi”

VIDEO:

Top Post Ad

Below Post Ad