Walimu pamoja na wafanyakazi wakiume katika shule ya Sekondari ya wasichana Moi jijini Nairobi wametakiwa kufanyikwa uchunguzi wa vinasaba ‘DNA’ ili kubaini watuhumiwa wa tukio la ubakaji lililofanyika shuleni hapo.
Polisi wamewaagiza walimu hao wa kiume, pamoja na wafanyakazi wanaoishi ndani ya shule hiyo kutekeleza zoezi hilo litakalosaidia kurahisha uchunguzi wa nani mtuhumiwa kwani taarifa zinasema hakuna mgeni aliyeingia usiku ule zaidi ya watu wa shuleni hapo.
“Uchunguzi huo wa ‘DNA’ utarahisisha kubaini watuhumiwa waliotenda tukio hilo la unyanyasaji wa kijinsia kwa mabinti hao kwani vipimo vya awali vya mabinti vimehifadhiwa”, imesema taarifa ya Polisi.
Gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa tayari maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha uhalifu na mkemia wa serikali hapo jana Jumatatu walichukua sampuli za wafanyakazi wanane wa shule hiyo miongoni mwao walimu 6 ili kufanyiwa ukaguzi wa maabara