Wamiliki wa Magari Wapewa Onyo Kali na Jeshi la Polisi

Wamiliki wa Magari Wapewa Onyo Kali na Jeshi la Polisi
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Fortunatus Muslim amefunguka na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kuwapa magari yao madereva wasiokuwa na leseni kwani endapo watabainika watakuwa wamejiingiza katika kosa la uvunjifu wa sheria za barabarani.


Muslim ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha East Africa Drive kilichorushwa jana jioni Juni 05, 2018 kutoka East Africa Radio baada ya kuwepo kadhia hiyo kwa watu wengi kupenda kuendesha magari ya watu bila ya kuwa na leseni inayowaruhusu kufanya hivyo huku wengine kutumia kigezo hicho kutenda uhalifu.

"Ni kosa kumpa gari dereva kuendesha wakati unajua kwamba hana leseni na hili kosa huwa linakuja mpaka kwa mmiliki wa gari kwa hiyo wote wawili watakuwa watuhumiwa kwaajili ya mujibu wa sheria", amesema Kamanda Muslim.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad