Wanajeshi wa Uganda Wawakamata Polisi wa Kenya na Kuwasweka Rumande

Wanajeshi wa Uganda Wawakamata Polisi wa Kenya na Kuwasweka Rumande
Wanajeshi wa Uganda wanawashikilia maofisa usalama watatu wa Kenya katika kile kinachoonekana ni utata unaozingira haki ya uvuvi kwenye Ziwa Victoria.

Maofisa hao walikamatwa na kupokonywa silaha na wanajeshi wa UPDF Jumatatu karibu na Mageta na Kisiwa cha Hama ndani ya Ziwa Victoria na walipelekwa katika nchi kavu jirani kwa kutumia boti.

Mashuhuda waliliambia gazeti la Nation kwamba maofisa hao walipokonywa bunduki na simu zao kabla ya kupeleka gereza la Bugiri nchini Uganda majira ya saa 12:00 jioni.

Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Siaya Patrick Lumumba alisema mkasa huo uliotokea saa 9:00 alasiri uliwahusisha wanajeshi wanane waliokuwa kwenye gari la doria.

Maofisa, alisema walizingirwa na wakawekwa pamoja na wavuvi wa Kenya waliokutwa wakivua samaki kwenye eneo la Uganda.

Lumumba alisema washambuliaji, walikuwa wamejihami kwa silaha nzito, kwanza waliteka boti tano na wakachukua injini zao.

"Maofisa wetu walizidiwa na washambuliaji waliokuwa wamejihami kwa silaha walioweka mtego wa kuvizia wakidhani ni raia na wavuvi,” alisema Lumumba.

Kamishna wa Mkoa wa Nyanza Moffat Kangi alipanga kwenda kujaribu kupata ufumbuzi wake.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad