Wanawake Mungu Anawaona...Ona Huyu Mwanamke Alichomfanyia Mmewe Mpaka Kapatwa na Kizunguzungu Cha Ghafla


Jamaa kaamka asubuhi, kavaa track suit na kumuamsha mkewe!

MUME: Amka twende jogging mke wangu?

MKE: Alaaa kwa hiyo una maana mi tipwatipwa?

MUME: Hapana si hivyo jogging ni nzuri kwa afya.

MKE: Kwa hiyo una maana mi mgonjwa?

MUME: Basi yaishe endelea kulala🤗
MKE: Kwa hiyo unaniona mi mvivu sana sio?

MUME: Hujanielewa mpenzi wangu sikuwa na maana hiyo baby

MKE: Kwa hiyo mie mjinga mpaka nashindwa kukuelewa?

MUME: Jamani mi sijasema hilo

MKE: Kwa hiyo mie muongo?

MUME: Chonde tusiendeleze haya asubuhi namna hii

MKE: Kwa hiyo mie ndio naendeleza ugomvi?

MUME: Sikia we lala mie naenda jogging.
MKE: Ndio zako hizo mambo yote unafanya peke yako hunishirikishi"🤐

MUME: Unajua nimeanza kusikia kizunguzungu
MKE: Unaona nikiongea kidogo unakimbilia kuumwa, mbinafsi sana wewe...

MUME: Basi ngoja tu nilale siendi jogging
Mke: Kwahiyo ulikua unanijaribu?


Wanawake Mungu anawaona

*NDIO MAANA WANAUME TUNAKUFA MAPEMA NA KUWAACHA WENGI MKIWA WAJANE*

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad