Wanawake Tuna Roho Mbaya - Linah Sanga

Wanawake tuna roho mbaya - Linah Sanga
Msanii wa bongo flava Linah Sanga, amesema wanamuziki wa kike wana wivu sana ndio maana hawapeani ushirikiano wa kutosha katika kazi kitu kinachopelekea wao kutoendelea.


Akizungumza na www.eatv.tv, Linah ameeleza kuwa wanamuziki wa kike wanashindwa kusaidiana kwasababu wanaogopa kuzidiana, na pia wanaona kwamba mmoja akimsaidia mwingine ataonekana anamkubali sana hivyo inapelekea kila moja kutaka kufanya kazi kivyake.

Linah ameendelea kusema tatizo hili ndio linapelekea kuwa na wasanii wakike wachache sana katika soko la muziki, kwasababu hata wale waliotangulia kuingia kwenye tasnia hiyo wanakuwa wagumu kusaidia wengine wakihisi kwamba ndio itakuwa chanzo cha kushuka kwao kimuziki.

“Wanawake tumeumbiwa wivu na roho mbaya ndio maana mtu anaona akimsaidia mwenzei atakuwa bora zaidi yake, na pale mtu anapoamua kukusaidia basi inakuwa ni kinafiki kwasababu nayeye atahitaji msaada wako”, amesema Linah.

Linah amewashauri wanawake wenzie kuungana na kuwa kitu kimoja ili waweze kupeleka muziki wao mbali,aliongeza kuwa upendo ni bora sana katika kazi na wasiishi kwa kuogopana.

Top Post Ad

Below Post Ad