Wapandishwa Kizimbani kwa Kughushi Risiti za Mashine za Kieletroniki

Wapandishwa Kizimbani kwa Kughushi Risiti za Mashine za Kieletroniki
Wafanyabiashara wanne na mkulima mmoja wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka tisa ya kughushi risiti za mashine za kieletroniki (EFD) za kampuni mbalimbali.

Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa leo Juni 28, 2018 mbele ya hakimu Augustine Ruizile amewataja  washtakiwa hao kuwa ni   Cost Nsolo (23) mkazi wa Mbagala, Monica Manase Mnuna (34) mkazi wa Kimara, Sumo Laurent Njige (45) mkazi wa Kimara, Maulid Ally  Mchila (38) mkazi wa Kigamboni pamoja na Brian Paul Minja (43) mkulima na mkazi wa Tabata.

Baada ya Msigwa kusomewa mashtaka hayo washtakiwa wote waliyakana na upande wa mashtaka ulidai  kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Ruizile alitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa hao, kutaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mdhamini atasaini bondi ya Sh 5 milioni.

Washtakiwa walikamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa huru. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 13,2018.



Tags

Top Post Ad

Below Post Ad