Wapotezaji paspoti waanza kuchunguzwa


NA FATUMA MUNA
Idara ya Uhamiaji nchini imeanza kufanya uchunguzi ili kuwabaini watu wanaoonekana kupoteza hati za kusafiria mara kwa mara na kuonya kwamba, watakaobainika hawatapewa tena hati hizo.


Kauli hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Idara hiyo, Mrakibu Ali Mtanda, ambaye amesema katika siku za hivi karibuni, kumekua na wimbi la baadhi ya watu kudai wamepoteza hati hizo ambazo baadhi yake zimeonekana zikitumiwa na watu wa mataifa mengine hali ambayo ni hatari kwa usalama wa nchi.

 Amefafanua kwamba, hati za kusafiria zinatolewa kwa mujibu wa sheria ya pasipoti sura 42 ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2004 na kufanyiwa marejeo mwaka 2018 ambapo pasipoti imetajwa kama nyaraka muhimu ambayo inatolewa kwa raia wa Tanzania.

Ameongeza kwamba wameweka gharama la shilingi laki tano kama faini ya kupata hati nyingine kulingana na unyeti wa hati hiyo.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad