Wasanii wa China na Tanzania Kubadilishana Uzoefu

Wasanii wa China na Tanzania Kubadilishana Uzoefu
Serikali ya Nchini china kupitia Wizara ya Utamaduni na Utalii imeamua kutoa fulsa kwa wasanii wa Tanzania na China  kwa ajili ya kubadirishana ujuzi wao kupitia warsha ya siku mbili iliyoandaliwa.

Mkurugenzi wa kituo cha Utamaduni wa China, Gao Wei amefunguka kuhusu warsha hiyo na  akusema kuwa wasanii hao wataongeza uzalishaji wa kazi za mikono na watajifunza mambo mbalimbali ambayo kwa nchi hizo mbili zitakapoweza kuonyesha ujuzi wao.

Ofisa utamaduni mkuu kutoka Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Habibu Msammy amesema kukutana kwa wasanii hao si tu kutaongeza uzoefu bali thamani ya bidhaa zao ili ziweze kuuzika kimataifa.

"Bidhaa itakapokuwa nzuri na yenye thamani itauzwa popote pale duniani, kwa hiyo tumieni warsha hii kujifunza vingi msivyovijua kutoka kwa wenzetu wa China ili kukuza sekta hii ya sanaa za mikono," amesema.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad