Watanzania 109 Waliokamatwa Kenya kwa Uvuvi haramu wameachiwa


Leo June 27, 2018 Kutoka Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni kuhusu Watanzania 109 waliokamatwa hivi karibuni kwa madai ya kufanya uvuvi haramu Bahari ya Hindi, upande wa Kenya wamepata dhamana na kurejea nchini.

Hata hivyo, bado Serikali za pande zote mbili zinaendelea kufanya mawasiliano jinsi ya kulishughulikia suala hilo.

Wavuvi hao walikamatwa eneo la Shimoni, linalomilikiwa na bandari Kusini Mashariki mwa Kenya karibu na mpaka wa Tanzania na kufikishwa mahakama ya Kaunti ya Kwale mwanzoni wa mwezi huu.

Walizuiliwa baada ya kushindwa kulipa dhamana ya Ksh20,000 (450000) kila mmoja.

Tangu wakati huo Serikali ya Tanzania imesema imeanza harakati za kuhakikisha kuwa raia hao wanaachiwa huru.

Top Post Ad

Below Post Ad