Watanzania Wawili Wanyakua Tuzo za Malikia Elizabeth

Watanzania Wawili Wanyakua Tuzo za Malikia Elizabeth
Vijana wawili kutoka Tanzania wametwaa tuzo ya Malkia Elizabeth ya viongozi vijana, ambayo hutolewa kwa vijana wenye uwezo wa kubadilisha jamii katika nyanja za kijamii, kielimu na utamaduni na kuleta maendeleo kupitia kazi zao.

Alice Magaka na Isaya Yunge, wameiwakilisha Tanzania katika tuzo hizo ambazo hafla yake imefanyika jijini, London nchini Uingereza, huku lengo lake likiwa ni kuona na kutambua namna vijana wanavyofanya kazi za kuzibadili jamii wanazotoka katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii na utamaduni.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyokutanisha vijana kutoka mataifa 38 yaliyo katika jumuiya ya madola, Malkia Elizabeth amesema kuwa tuzo hizo ni kwa ajili ya kutambua na kuthamini uwezo wa vijana wanaoweza kufanya vitu vikubwa katika jamii, wakiwa na umri mdogo.

“Vijana hawa tunawapa tuzo hizi ili kuamsha hamasa kwa vijana wengine kujitolea katika jamii, kubadili mitazamo hasi, kuleta mafanikio chanya na kukuza uchumi usiokuwa tegemezi katika mataifa yao”, amesema Malkia Elizabeth.

Alice amepokea tuzo hiyo kupitia  kwa kazi anayofanya ya kuelimisha wasichana kuhusu usafi wakati wa hedhi na kutoa huduma ya kugawa taulo za kike kupitia kampeni anazofanya ili kupata michango kutoka kwa jamii, huku Isaya amepokea kwa ugunduzi wa  programu ya simu, SomaApp, programu ya simu ambayo inasaidia kurahisiaha usomaji kwa wanafunzi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad