Watu Wanaonichamba na Kunisema Kuhusu Dogo Janja Wivu tu Unawasumbua- Irene Uwoya

Watu Wanaonichamba na Kunisema Kuhusu Dogo Janja Wivu tu Unawasumbua-Irene Uwoya
STAA wa Filamu za Kibongo, Irene Uwoya amedai kuwa watu wanaomchamba ‘kumsema vibaya’kuwa hakustahili kuolewa na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ ni wivu ndio unawasumbua kwani wapo ambao waliitamani nafasi hiyo.



Akipiga stori na Udaku wa Mjini Uwoya alisema kuwa kuna wengine wanashangaa kwa nini ameolewa na mwanamuziki huyo lakini yeye haimshitui kwani alishaziba masikio yake siku nyingi tangu alipoamua kumpenda Dogo Janja.



“Unajua kuolewa ni heshima ambayo wanawake wengi wanaihitaji, kuna ambao wananisema vibaya kwa wivu, walitamani wao ndiyo waolewe lakini imeshindikana ndiyo wananisema vibaya, wala sijali, nafurahia maisha yangu ya ndoa na wala sina habari yoyote,” alisema Uwoya.

Top Post Ad

Below Post Ad