Jana June 5, 2018 stori kutoka Jeshi la Polisi mkoani Mara limewatia mbaroni watu watatu kwa tuhuma za kuwapa sumu simba tisa katika mbuga ya Serengeti.
Inaelezwa kuwa maafisa wa mbuga ya Serengeti waligundua mizoga ya simba wikiendi iliyopita na walikuta watuhumiwa hao wamewakata mikia na miguu simba hao na kuondoka nayo.
Msemaji wa Hifadhi ya Taifa Pascal Shalutete amesema kuwa waligundua vifo vya simba hao baada ya kula mizoga ya ng’ombe waliokuwa wakifugwa kandokando ya hifadhi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mbuga ya wanyama ya Serengeti ndio mbuga kubwa na mashuhuri nchini Tanzania ikiwa na kilomita zaidi ya elfu 14 huku kwa mwaka ikitajwa kutembelewa na watalii zaidi ya laki tatu na nusu.
Aidha watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.