Watuhumiwa 28 Wanaosafirisha Watoto kwa Magendo Wakamatwa

Watuhumiwa 28 Wakamatwa kwa Kusafirisha Watoto Kimagendo
Shirika la polisi la EU limetangaza siku ya Ijumaa kuwa watuhumiwa 28 wamekamatwa nchini Uhispania kwa makosa ya kuwapitisha watoto kimagendo kutoka Morocco hadi Ulaya.
Katika operesheni hiyo Europol imetoa taarifa hiyo kuwa watuhumiwa 28 wamekamatwa kwa kuwasafirisha kimagendo watoto kueleka Ulaya.
Watuhumiwa wanaaminika kuwa waliwachukua watoto wadogo 100 kutoka Morocco hadi Uhispania na kisha kukamatwa nchini Hispania.
Europol pia imesema kuwa watoto walipelekwa Ulaya kwa € 2,000 (dola 2,330) hadi € 8,000 (dola 9,320) na waliingia Uhispania kinyume cha sheria kwa njia za hatari za usafiri kama vile boti za mbao, jet skis au boti za uvuvi au kwa magari na malori .
Aidha, polisi wamekamata nyaraka bandia, vifaa vya kuhifadhi data na simu za mkononi katika uendeshaji huo.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad