“Wauza Unga Wanapata Tabu Sana” – Kamishna Siang’a

Katika kufanikisha mapambano, dhidi ya wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya nchini, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Siang'a amesema kuwa wamefanikiwa kupunguza uingizwaji wa dawa hizo nchini.

Akizungumza na www.eatv.tv Kamishna Siang’a amesema kuwa katika utumishi wake wa mwaka mmoja tangu alipoteuliwa na Rais Magufuli, amefanikiwa kupunguza mitandao ya iliyokuwa ikiingiza madawa kutoka Asia na Afghanistan.

“Dawa aina za Heroin tumefanikiwa kupambana nazo kwa kiasi kikubwa kwani ndio zilizokuwa zikiongoza kwa madhara zaidi kwa vijana wetu na tumefanikiwa kuzuia kwa asilimia 90”, amesema Kamishna Siang’a.

Kamishna Siang’a ametaja pia sababu ya wafanyabiashara hao kutumia zaidi wanawake kubeba dawa hizo, kuwa sababu kuu ni uwezo wa tumbo la mwanamke kubeba mzigo mkubwa zaidi ya mwanaume na njia nyingine zilizokuwa zikitumika zaidi ni usafiri wa baharini hasa mashua.

Hayo yamejiri ikiwa leo, ni maadhimisho ya kupambana na Dawa za kulevya Duniani, ambapo Kitaifa yamefanyika mkoani Iringa, yakiongozwa na kauli mbiu ‘Tujenge maisha yetu, Jamii yetu na utu wetu, bila dawa za kulevya’. Msikilize hapo chini Kamishna Siang’a amefunguka zaidi.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad