Waziri wa Sheria, Phillip Lee ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo akipinga “kusudio la serikali kudhibiti” jukumu la Bunge kushughulikia mpango wowote wa mwisho kuhusu Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya (Brexit).
“Sababu hasa ya kuchukua uamuzi huu sasa ni mchakato wa Brexit na kusudio la serikali kutaka kuzuia jukumu la Bunge kuchangia katika matokeo ya mwisho ya kura inayofanyika leo,” alisema kupitia tovuti yake.
Alisema, 'Ikiwa siku zijazo, nitakaa kuwaangalia machoni watoto wangu na kusema ukweli mtupu nilifanya kitu gani bora kwa ajili yao siwezi, kwa dhamira safi kuunga mkono hicho kinachofanywa na nchi yetu kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya kama inavyoshughulikiwa.”
Kujiondoa huko kulikotangazwa na Lee katika kikao cha watu mashuhuri jijini London ni pigo kubwa kwa Waziri Mkuu Theresa May wakati huu anapokabiliwa na mfululizo wa kura juu ya Muswada wa Uingereza Kujiondoa EU.
Lee, alisema anaamini sera ya Uingereza kujiondoa ina “madhara” kwa nchi.
Huku kukiwa na fununu ya mawaziri wengine kujiuzulu, aliwataka wabunge wa Chama cha Conservative kuweka shinikizo iandaliwe kura ya maana juu ya mpango wa Brexit na akapendekeza iandaliwe kura ya pili ya maoni kuhusu Brexit.