Waziri mkuu wa New Zealnd Jacinda Ardern amejifungua mtoto wake wa kwanza wa kiki wa uzani wa kilo 3.31.
Hii inamfanya awe kiongozi wa pili katika historia aliye madarakani kujifungua mtoto.
Bi Ardern alilazwa kwenye hospitali moja mjini Auckland siku ya alhamisi.
Mbali na kuwa Kiongozi wa pili katika historia kujifungua akiwa uongozoni, ni waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi kuliongoza New Zealand tangu 1856.
Bi Ardern mwenye umri wa miaka 37 atachukua mapumziko kwa muda wa wiki sita huku Naibu wake, Winston Peters akichukua usukani.
Hata hivyo ushauri wake utahitajika kwa baadhi ya masuala muhimu ikiwemo kusoma kumbukumbu ya mkutano wa mawaziri licha ya kuwa likizoni.
"Niko na hakika tunapitia hisia nyingi zinazopitiwa na wazazi wengine pia, na vile vile tunatoa shukrani kwa ukarimu na taarifa za pongezi kutoka watu wengi. Asanteni." Aliongeza kwneye taarifa aliyotoa.
Bi Ardern, ambaye alichaguliwa mwezi Oktoba mwaka uliopita, alitangaza Januari mwaka huu kuwa yeye na mpenzi wake Clarke Gayford walitarajia mtoto.
"Mimi sio mwanamke wa kwanza kuwa na majukumu mengi. Mimi sio mwanamke wa kwanza kufanya kazi nikiwa na mtoto. Kuna wanawake wengi walionitangulia katika hili, "
Mwingine kujifungua uongozini ni waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto, aliyejifungua mtoto wa kike mnamo mwaka 1990.
Alikuwa kiongozi wa kwanza kujifungua akiwa ofisini.