Waziri Mwijage Aipongeza Kampuni Ya Total Kwa Kuzindua Mafuta Ya Magari Rafiki Kwa Mazingira

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ameipongeza kampuni ya mafuta ya TOTAL kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuhakikisha kuwa watanzania wanapata mafuta bora ya vyombo vya moto.

Mwijage alizungumza jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa mafuta ya vyombo vya moto aina ya TOTAL Excellium kutoka kampuni ya mafuta ya TOTAL. Mafuta hayo yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya ubora wa juu ya kimataifa ya TOTAL EXCELLIUM, kwa bidhaa zinazotumia mafuta ya Petroli na Diesel katika soko la Tanzania.

“Uzinduzi wa mafuta haya umekuja wakati muafaka kwani sasa tuko kwenye wiki ya mazingira na mafuta haya yanapunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na vyombo vya moto, nawapongeza kampuni ya TOTAL kwa kuwaletea watanzania bidhaa bora, na mimi na utaalamu wangu wa mafuta nafahamu hii ni hatua kubwa sana kwenye teknolojia ya kuboresha mafuta,” alisema Mwijage.

Mafuta haya mapya yana uwezo wa kusafisha injini na kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu, kuwezesha matumizi kidogo ya mafuta na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na moshi wa vyombo vya moto.

Mafuta ya TOTAL EXCELLIUM yanapatikana katika vituo vyote vya kuuza mafuta vya kampuni ya TOTAL kwa gharama ya bei ya kawaida ya mafuta kwenye soko.

Tarik Moufaddal, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya TOTAL nchini anasisitiza, “Kuzinduliwa kwa TOTAL EXCELLIUM, katika soko la Tanzania ni hatua mpya na muhimu kwetu nchini hususani katika kufanikisha dhamira yetu ya kuingiza bidhaa bora za nishati. Tunayo dhamira ya kuwapatia wateja wetu bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, sambamba na huduma bora kupitia mtandao wetu ambao umeenea nchini kote, uzinduzi wa TOTAL EXCELLIUM, unadhihirisha kuwa tumejipanga kuleta mapinduzi yenye kuleta manufaa katika sekta ya mafuta nchini.”

“TOTAL EXCELLIUM imetengenezwa kwa teknolojia ya juu ya kisasa ambayo inawezesha kusafisha injini, kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu bila kuchoka, matumizi kidogo ya mafuta kuendesha injini, kupunguza uchafuzi wa mazingira utokanao na moshi na ni mazuri kwa matumzi ya aina zote za magari kuanzia madogo mpaka makubwa,” aliongeza Tarik.

“Uzinduzi huu ni moja ya ubunifu mkubwa wa kampuni uliolenga kuhakikisha wateja wetu wanapata bidhaa bora na kuwawezesha matumizi kidogo ya mafuta yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ya Excellium.

"TOTAL EXCELLIUM imetengenezwa kwa ubunifu wa teknolojia za kisasa zenye kuleta ubora. Timu yetu ya wataalamu wa utafiti wamefanikisha kutengeneza mafuta haya kukidhi mahitaji ya wateja wetu wanaotumia magari ya kisasa ambayo yanahitaji umakini mkubwa katika matunzo ya injini kwa matumizi yao ya kila siku”  Mkurugenzi wa Mtandao wa TOTAL wa Nikesh Mehta.

“Zaidi ya watafiti makini na wataalamu wenye uzoefu mbalimbali wanafanyia kazi suala la kuleta bidhaa za mafuta na vilainishi vya injini na mitambo zenye ubora mkubwa zaidi katika kituo chetu cha utafiti cha Solaize,nchini Ufaransa.Wataalamu hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka miwili kuboresha mafuta ya TOTAL EXCELLIUM.

"Zaidi ya kanuni za kisayansi 2,300 zimefanyiwa majaribio katika maabara kwa zaidi ya masaa 6,000 na mafuta haya yamefanyiwa majaribio ya awali barabarani kwa zaidi ya masaa 8,500 sawa na kilometa 300,000.

"Haya yote yanathibitisha uhakika na ubora wa mafuta ya TOTAL EXCELLIUM na yanasafisha injini za magari na kupunguza uharibifu wa mazingira,” anasema Marsha Msuya, Mkurugenzi wa Masuala ya Ndani ya kampuni ya TOTAL.

Credit: Fullshangwe

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad