Kwaya moja ya Wanafunzi wa kike nchini Afrika Kusini imezua gumzo nnchini humo baada ya wanakwaya wake kutumbuiza katika jukwaa la tamasha la EC Choral lililofanyika Jumatatu ya Mei 28, 2018.
Waziri wa Elimu nchini Afrika Kusini, Bi. Angie Motshekga
Wanafunzi hao ambao hata hivyo hawajabainika wanatoka shule gani, na mpaka sasa video yao imezua gumzo nchini humo baada ya kusambaa mitandaoni.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Dispatch limedai kuwa mwalimu wa kwaya hiyo ya wanafunzi ambaye hakujitambulisha jina lake alijivunia kuona wanafunzi hao wakienzi utamaduni na mila za kabila la Xhosa.
“Hili ni jambo la furaha kwetu sisi kama wa Xhosa, watoto wetu wanakua katika mazingira ya kisasa hadi wanasahau tamaduni zao nadhani sasa tunarudisha utamaduni wetu wa enzi hizo unaoonekana kusahaulika,“ameeleza Mwalimu huyo.
Wasichana hao kwenye video hiyo ambao kifuani wanaonekana kuwa watupu huku kiunoni wakivalia vinguo vifupi. video yao imezua gumzo kiasi kwamba serikali nchini kupitia Wizara ya Elimu kuingilia kati.
Waziri wa Elimu nchini Afrika Kusini, Angie Motshekga amelaani tukio hilo na kuliagiza Jeshi la Polisi nchini humo kufanya upelelezi juu ya video hiyo ili kuwabaini wahusika hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la habari la AFP.
“Huu ni udhalilishaji wa kijinsia na kinyume cha maadili ya taifa letu, hakuna makosa kupenda tamaduni wako lakini hakukuwa na umuhimu wowote kucheza wakiwa wakiwa utupu”.amesema Bi. Angie Motshekga.
Tazama video ya wanafunzi hao wakitumbuiza (video by Dispatch Live).