Maamuzi hayo ya Waziri Kamwele yamekuja leo Jumatatu, Juni 18 baada ya serikali kupokea taarifa za kuwepo kwa udanganyifu katika mradi huo ambapo mbali na ubadhirifu uliogundulika pia upo udanganyifu wa idadi ya visima vilivyokamilika kama ambavyo taarifa zilizowasilishwa wizarani na DAWASA na uhalisia katika eneo la utekelezaji miradi.
Aidha Taarifa ya Waziri Kamwele imesema kuwa kutokana na kuwa Mhandisi Mwang'ingo ndiye aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa mradi huo kwa niaba ya DAWASA na seerikali basi anatengua nafasi yae hiyo ili kupisha uchunguzi wa TAKUKURU.
Aidha Waziri amemteua Dkt. Sufian Masasa kukaimu nafasi hiyo mpaka utaratibu mwingine utakapokamilika.
Pamoja na hayo Waziri Kamwele amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA kwa kushindwa kuchukua hatua mapema katika kunusuru mradi huo.