Wolper Afunguka Mahusiano Yake na Mr Nice

Wolper Afunguka Mahusiano Yake na Mr Nice
BAADA ya kuonekana akila bata nchini Kenya na mwanamuziki Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ na kuibuka kwa madai kwamba wanatoka kimapenzi, staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameibuka na kufungukia ukaribu wao.

Awali Wolper aliweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha akila bata yaani wakiwa klabu akivuta shisha huku Nice akinywa pombe ambapo watu mbalimbali walidai huenda wanatoka kimapenzi.

Kutokana na madai hayo Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Wolper kwa njia ya simu akiwa nchini Kenya na kumuuliza kuhusu ukaribu wake na Nice ambapo alisema ni wa kawaida tu na wako karibu kwa sababu bosi wao ni mmoja.
Image result for wolper na mr nice
“Watu wajue sisi tupo kikazi zaidi kwani kuonekana na mtu ni lazima awe mpenzi wako? Si lazima, huyu ni kaka yangu na bosi wetu ni mmoja, projekti yetu ikiwa tayari tutaitangaza itajulikana tu lakini kwa sasa bado ni mapema kuitangaza,” alisema Wolper.

Wolper kwa sasa yupo nchini Kenya ambapo anafanya kazi zake za ufundi wa cherehani na ndipo alipokutana na msanii Mr.Nice.

Top Post Ad

Below Post Ad