Wolper ataja vitu viwili vinavyomtesa katika mapenzi


Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ametaja vitu viwili ambayo humtesa katika mahusiano.

Mrembo huyo ambaye kwa sasa amejikita katika Ubunifu wa Mavazi, katika mahojiano na Wasafi TV amesema muda na uongo ni vitu vinavyomtesa.

“Kitu kinachonitesa na kunipa stress kwenye kwenye mahusiano ni uongo na muda. Nafanya sana kazi lakini nahitaji sana muda wa kuwa na mtu wangu, kwa hiyo uongo na muda ni tatizo sana kwenye mahusiano,” amesema.

“Mtu akiaanza kunidanganya au kunipa muda mchache wa kuwa naye na kuwa out of mood kabisa na ninaweza nikaamka nikamwambia it’s over bila kujali chochote,” amesisitiza.

Hata hivyo ameeleza kuwa kuna uongo ambao anauhitaji; ‘Uongo ninaouhitaji mimi ni ule kunidanganya kuwa unanipenda, tangu nizaliwe sijawahi kuona mwanamke mzuri kama wewe, huo ndio uongo unahitajika kwa kila mwanamke,’.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad