Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuivusha Yanga wakati huu wa mpito, Abass Tarimba, amesema kuwa ipo kwenye mkakati wa kuleta wachezaji wenye ubora zaidi.
Kutkana na mwenendo wa klabu na Yanga kutoridhisha hivi sasa, Tarimba amefunguka na kusema inabidi klabu ilete wachezaji watakaokuwa na uwezo mkubwa zaidi ya waliopo sasa.
Mwenyekiti huyo wa kamati ya mpito, amesema inafikia hatua Yanga iwe na wachezaji wenye majina makubwa kuizidi klabu ili waweze kuipa timu matokeo chanya.
Tarimba amezungumza hayo wakati wachezaji wote wa kikosi hicho wakiwa mapumziko na mwezi ujao wanatarajia kukutana tena kambini.
Yanga watakuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC dhidi ya Gor Mahia FC jijini Nairobi utakaopigwa Julai 18 2018.