Yanga Yaiomba TFF Kujitoa Mashindano ya Kagame CUP

Yanga Yaiomba TFF Kujitoa Mashindano ya Kagame CUP
Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Yanga umewaandikia barua TFF kuwaomba kujitoa katika mashindano ya Kagame CUP yanayotarajiwa kuanza June 28 mpaka Julai 13 2018 jijini Dar es Salaam.


Sababu za msinngi zilizofikia Yanga kuandika barua hiyo ni kufanya maandalizi ya michunao ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18 jijini Nairobi.

Kutokana na muingiliano wa ratiba ya KAGAME na CAF, Yanga wameona ni vema kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya tatu baada ya kucheza na USM Alger pia Rayon Sports ya Rwanda.

Taarifa hizo zinazoelezwa kutoka Yanga kupitia viongozi wa Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo, wameazimia kufanya maamuzi hayo ili kuepuka kubanwa na muingiliano wa ratiba hiyo ambayo imekuwa si rafiki kwao.

Kufuatia kuandika barua hiyo ya kuomba kujiondoa, Yanga wanakuwa wameikwepa Simba kwenye mashindano ambapo walikuwa wamepangwa pamoja na mabingwa hao wa Ligi Kuu Vodacom.

Simba na Yanga zimepangwa pamoja kwenye kundi C ambapo kuna timu zingine ambazo ni Dakadaha ya Somalia pamoja na St. George kutoka Ethiopia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad