Zitto alia bajeti kuwaumiza wakulima, wafanyakazi

Zitto alia bajeti kuwaumiza wakulima, wafanyakazi
Chama cha ACT Wazalendo, kimesema, Bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha 2018/19, inawaumiza wafanyakazi na wakulima nchini.


Leo wakati akifanya uchambuzi wa Bajeti hiyo, mbele ya waandishi wa habari, na wadau wengine wa uchumi na biashara, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema, utekelezaji wa Bajeti hiyo utapungua kwa 23% huku wakulima na wafanyakazi wakiendelea kuumia.

Kiongozi huyo amesema ili kuwapa unafuu amependekeza Kodi ya Mshahara yaani Paye, ipunguzwe na michango kwenye mifuko ya jamii ifanyiwe marekebisho ikiwemo kushushwa kwa michango ya pensheni kutoka 20% mpaka 12% ili kuwapa unafuu wafanyakazi na waajiri.

 Kuhusu kilimo, amesema, Bajeti yake imepunguzwa kwa 23% licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi, huku kikiajiri 66% ya Watanzania wote.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad