Mwaka 2014 kulikuwa na habari kwamba rapa Earl Hayes alimshtumu mkewe kutoka kimapenzi na muimbaji Trey Songz wakati wakiwa kwenye ndoa.
Suala hili lilipelekea Earl Hayes kumuua mke wake na baadae naye akajiua lakini sasa 50 Cents ameibuka na kusema kwamba Mayweather ndiye alikuwa chanzo cha tukio hilo na sio Treys kama ilivyosemwa.
Hayes alikuwa msanii aliyekuwa chini ya lebo ya Mayweather na 50 amesema wawili hao walikuwa wakiongea bila Hayes kujua kwamba Mayweather anamzunguka kwa kutembea na mke wake.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram 50 Cents amemuambia Mayweather aeleze chanzo cha kifo cha Stephanie na aeleze kwanini walikuwa wakiwasiliana na Hayes wakati mauaji hayo yakitokea.
50 Cents amekwenda mbali zaidi na kusisitiza kwamba Mayweather alikuwa ndiye anapandikiza story kuhusu Mayweather kuhusika na vifo hivyo ili kifunika ukweli kuhusu yeye.
Katika hali nyingine Mayweather amemtupia diss 50 kwa kusema kwamba utajiri wa msanii huyo ni $20m wakati yeye Floyd Mayweather anamiliki saa yenye thamani ya $18m.
Pia Mayweather amewaomba mashabiki wake kumponda 50 Cents kwa kuandika maoni wakimuhusisha na panya na washindi 9 watapata $1000 karibia milioni 2.5 za Kitanzania.
Nini chanzo cha bifu hili?
Miaka ya 2012 Mayweather na 50 Cents walionekana kuwa marafiki, lakini kwa mara kadhaaa wamekuwa wakikwaruzana na baadae bifu lao kuonekana kuisha.
Lakini chanzo haswa safari hii ni saa ambayo Mayweather alipost “billionaire watch” ambayo alidai ina thamani ya $18m hali ambayo ilimpelekea 50 kuponda juu ya hilo.
50 alimuambia Mayweather ni mjinga ndio maana anadanganywa kuhusu thamani ya vitu na hii ilimchukiza Maywether ndipo vita vya maneno kati ya wawili hawa ikaanza upya.