Amnesty International imelaani mamlaka nchini Iran kwa kumchapa viboko hadharania mwanamume ambaye alipatikana na hatia ya kunywa pombe wakati alikuwa na umri wa miaka 14.
Vyombo vya habari vilichapisha picha za mwanamume ambaye alitambuliwa kama "M R" akichapwa viboko 80 kwenye mji ulio mashariki wa Kashmir siku ya Jumanne.
Waendesha mashtaka wanasema alikamatwa wakati wa maadhimisho ya mwaka wa Iran wa 1385 wa kati ya (Machi 2006 na Machi 2007) na alihukumiwa mwaka uliopita.
Wanaume waliofanya mapenzi wachapwa viboko 85 Indonesia
Wanafunzi wasulubiwa na kutandikwa viboko kwa kuchelewa
Haijulikani sababu iliyochangia adhabu hiyo kuchukua zaidi ya miaka 10 kutekelezwa.
Picha hizo zinaonyesha mwanamume akiwa amefungwa kwenye mti akichapwa na mtu ambaye amejifunika uso. Umati mdogo wa watu nao wanaonekana wakitazama kwa mbali.
Mwaka 2014 raia sita wa Iran walihukumiwa jela na viboko 91 baada ya kukamatwa baada ya kuonekana wakiuchezea densi wimbo wa Pharrel Williams.
Mambo yanayoweza kusababisha uchapwe viboko Iran
Uzinzi, kupiga busu hadharani, wizi, vitendo vinavyohusiana na mapenzi ya jinsia moja na kufuru yote hayo yanaweza kusababisha mtu kuchapwa viboko nchini Iran. Wale wanaoptikana na hatia uhukumiwa kati ya viboko 10 na 100 mgongoni kwa kutumia fimbo ya urefu wa futi tatu.