Agizo la vyeti, Kamanda Muslim apigiwa magoti


Mwenyekiti wa Kamati ya Madereva bodaboda Taifa,  Bw. Rashid Omar Faru ameitaka serikali kutazama namna ya kuwasaidia madereva bodaboda ambao wana vyeti  vilivyotolewa katika mafunzo ya muda mfupi kwa kuwa kinachozingatiwa ni dereva kufahamu sheria na alama za barabarani awapo kazini.


Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Taifa Fortnatus Muslim (Kushoto)

Kauli ya Mwenyekiti huyo imekuja ikiwa ni siku moja baada  ya Kamanda Muslimu kuweka wazi kwamba kutakuwa na Operesheni ya kukagua vyeti vya madereva wa mabasi, na wale wote ambao wanaendesha vyombo vya usafiri.

Akizungumza na www.eatv.tv, Bw. Faru ameeleza kuwa yeye kama Mwenyekiti wa Bodaboda Taifa, anafikiri kuwa madereva bodaboda kukaa darasani miezi 3 au zaidi hakumfanyi kuwa dereva mzuri kama tu atakuwa hajapatiwa mafunzo muhimu yahusuyo barabarani, na kufahamishwa lengo la mafunzo.

Bw. Faru amesisitiza kwamba kabla ya serikali haijaanza kutaka vyeti vya vyuo vya kuanzia miezi mitatu inapaswa kukumbuka kwamba, katika mafunzo ya wiki mbili mbili yaliyokuwa yakitolewa na Jeshi la polisi kwa kushirikiana na baadhi ya vyuo, ndivo ilitumika hata katika kupata leseni za udereva TRA.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo ameiomba serikali kushirikiana kwa ukaribu sana na Kamati zao kwa kuwa ndiyo walioshikilia dhamana ya madereva wa bajaji na bodaboda nchini, hivyo kabla ya kutoa matamko wangekuwa wanakutana kwanza ili kujadili hoja kama hiyo ya vyeti.

Pamoja na hayo amewaomba madereva kuhakikisha wanapata mafunzo ambayo yanatolewa ili wapate vyeti kuepusha usumbufu unaoweza kutokea kwa kuwa zamu yao kukaguliwa ipo mbali kutokana na jinsi operesheni inavyofanyika.

Akiwa katika kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa kupitia East Africa radio, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Taifa Fortnatus Muslim alisema "Kwa mujibu wa sheria za nchi, dereva anajifunza kuendesha usafiri kwa miezi mitatu na hakuna mafunzo ya wiki mbili halafu mtu unasema umeenda chuo, hapo utarudi chuo tu"

Kamanda Muslim alisema kuwa utaratibu wa kupata leseni ni kuanza masomo chuoni kwa miezi mitatu,na baada ya kutahiniwa na polisi kisha TRA ambao wanatoa leseni, na kwa kuuwisha (renew) ni baada ya miaka mitatu na dereva lazima aingie darasani kwa mafunzo kila anapotaka kuongeza daraja.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Enough is enough business as usual tumeichoka, watu wanakufa ovyo wengine wanaachwa walemavu kisa ajali barabarani. Maoni yangu, hata walio na vyeti wakahakikiwe kama kweli waliqualify au manuva. Hakuna huruma vyeti sio njugu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad