Ajali Yaua Watu Watano Mbeya Usiku wa Kuamkia Leo


Watu watano wanadaiwa kufariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali iliyohusisha lori pamoja na gari  dogo aina ya Noah eneo la mteremko wa mlima Igawilo nje kidogo ya jiji la Mbeya.

Ajali hiyo iliyohusisha magari matatu imetokea kwenye mteremko wa mlima Igawilo na kwa mujibu wa mashuhuda gari lenye kontena ililiangukia gari aina ya Noah iliyokuwa na abiria na inasadikiwa watu watano wamepoteza maisha.

Ajali hii imetokea ikiwa ni muda mfupi tu  baada ya Waziri Mpya wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kutembelea Mbeya na kutangaza kuvunja Baraza la Taifa la Usalama Barabarani pamoja na Kamati zake zote za Mikoa na Wilaya
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad