Ali Kiba Asajiliwa Rasmi Kuichezea Coastal Union, Kilichobaki ni Saini Yake Tu

Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga umethibitisha kutarajia kumsajili msanii wa muziki wa Bongo, Alikiba kwaajili kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Alikiba anayetamba na kibao chake cha Mvumo wa Radi huenda akaanza kuonekana kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu kupitia na timu yake ya Coastal Union endapo usajili huo utakamilika.

Kupitia kipindi cha Esports kinacho ruka kwenye radio ya E FM, Mwenyekiti wa klabu ya Coastal Union, Steven Mguto amethibitisha kuwa kwenye mazungumzo na msanii huyo ili kupata huduma yake ya kukipiga katika kikosi cha wagosi hao wa kaya.

"Kiukweli siku zimebaki kidogo lakini na sisi kama zoezi letu limefikia ukingoni nafikiri mpaka kesho tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kueleza nani na nani tumemsajili.

"Kwa sababu kwa sasa ndiyo tunamalizia watu wengine maswala ya mikataba sasa sirahisi kuweza kumtaja mkataba bado haja saini mwisho wasiku anaweza akageuza nia na ikawa kitu kingine.

"Kwa kiasi kidogo kuna ukweli wa kutaka kumsaini Alikiba lakini pia mambo haya jakaa sana sawa lakini wenyewe mnamuona naye ni mchezaji ingawaje si wa kiwango cha juu kwasababu hana mazoezi ya mara kwa mara ya kucheza mpira hivyo kuwa katika mazungumzo ni kweli.

Alikiba ataweza kuisaidia Coastal Union licha ya uchezaji ndani ya uwanja lakini pia ataweza kuibeba klabu hiyo kupitia umaarufu wa staa huyo wa muziki nchini na bara zima la Afrika.

Klabu ya Coastal Union imepanda rasmi ligi kuu mwaka huu baada ya kuiyaga michuano hiyo msimu wa mwaka 2015/16.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad