Akizungumza na Championi Ijumaa, meneja wa timu hiyo, Said Hilary alisema Ali Kiba ni mchezaji mzuri na ameenda kwenye timu ya mpira na lengo lao kubwa ni kuitangaza Coastal.
“Tumemsajili kwa mkataba wa mwaka mmoja na tunafahamu yeye ni mwanamuziki kwa hiyo akiwa na shughuli zake za kimuziki ataendelea na shughuli zake kama kawaida na akiwa yupo huru basi atacheza kuisaidia timu maana tuna uamini uwezo wake ndiyo maana tumemsajili,” alisema Hilary.
Na Isaya Mbena, Championi Ijumaa