Moja ya habari zilizosambaa sana katika mitandao ya kijamii leo ni habari ya msanii mkubwa tanzania, Diamond Platinumz kuzuiwa uwana wa ndege kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa hana kibali vcha kwenda kufanya show nje ya nchi.
Na hata baaada ya mamlaka husika iliyomzuia kuulizwa walisema kuwa wamefanya hivyo kwa diamond ili kuwafunza wanamuziki wengine kufuata utaratibu kuhusu sheria mpya za BASATA.Kila mtu alipokea kwa hisia zake swala hio na mmoja aliyelipokea kwa masikitiko ni msanii wa vichelesho nchini masanja mkandamiza ambae katika akaunt yake ya twitter aliandika
Diamond ni moja kati ya vijana wanaojituma sana ili kufanikiwa na kusaidia watu wengi kufanikiwa.huwezi kupendwa na kila mtu lakini hii sumu ya baadhi ya watanzania kufurahia mtu akipata tatizo au kumzushia upopompo anapofanikiwa au kuchukiwa mtu kupiga hatua inahitaji maombi ya kitaifa.