Anusurika kifo kwa kutaka kufanya wizi wa Mtandao


Na manuel kaminyoge,Songwe, 
Kijana mmoja aliyefahamika kama Lusekelo Mwanjala (22) amenusurika kifo kutoka kwa raia wenye hasira kali baada ya kubainika akitaka kufanya wizi kwa njia ya mtandao kwa wakala wa tigopesa katika mtaa wa ilolo  mamlaka ya mji mdogo vwawa wilayani mbozi mkoani songwe. 

Kuwepo kwa mawasiliano ya mitandao mbalilmbali kumelaisisha mawasiliano katika jamii lakini kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vibaya mitandao hiyo kwa udanganyifu na kuwatapeli watu  kwa Njia ya mitandao hiyo.. 

Majira ya asubuhi katika mamlaka ya  mji mdogo  vwawa hali haikuwa nzuri kwa kijana lusekelo mwanjala (22)  ambaye amenusilika kifo kutoka kwa raia wenye hasira kali baada ya kubainika akitaka kufanya wizi  na udanganyifu kwa  njia ya mtandao kwa wakala wa tigopesa. 

Kufuatia tukio hilo baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wa mamlaka ya vwawa wamesema kuwa wahalifu kama hao wachukuliwe hatua kali za kisheria huku wakitoa wito kwa jeshi la polisi kutowaachia huru watuhumiwa na utapeli. 

Kwa upande wake mwenyekiti  wa mamlaka ya mji mdogo wa vwawa  Ephrahim Mwakateba amewataka wafanyabiashara kuwa makini zaidi kwani matapeli wamekuwa wengi na wa aina mbalimbali huku afisa mtendaji wa kata ya ilolo Rehema Mwakilusya ametoa wito  kwa vjina kuachana na maswala ya wizi badala yake wajikite  kufanya kazi halali. 

Kwa upande wake  mkuu wa wilaya ya ileje ambaye ni kaimu mkuu wa wilaya ya mbozi Joseph Mkude amekemea uwepo wa wahalifu kama hao kwani wamekuwa wakiwaibia wananchi ikilinganishwa kuwa wengi wao hawana elimu juu ya  utapeli huo na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad