Aunty Ezekiel Acharukia Ishu ya Wema Sepetu na Zari

MREMBO anayejua kuzitendea haki sini za muvi za Kibongo, Aunt Ezekiel amewacharukia wanaomchokonoa mitandaoni kuhusu kuwa karibu na upande wa aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinan Hassan ‘Zari’ huku pia akiwa ni shosti wa karibu wa mrembo aliyewahi kuwa mpenzi wa Diamond, muigizaji Wema Sepetu.

Akizungumza na Amani juzikati, Aunt alisema majungu hayo yameanza mitandaoni baada ya kusikia amealikwa kwenda kwenye bethidei ya mtoto wa Zari, Tiffah inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao lakini kamwe majungu hayo hayamsumbui.

“Ifike mahali tufunge mjadala, kila siku ni Aunt kuwa karibu na Zari, Wema kama ni bethidei nitaenda tu. Hawa wote ni marafiki zangu sasa siwezi kubagua kwa kuwa eti Wema aliachana na Diamond wakati kule kwa kina Diamond pia kuna mpenzi wangu Iyobo na isitoshe Zari ni wifi yangu kwa upande mwingine,” alisema Aunt.

Stori: Imelda Mtema, Amani

GPL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad