Aunty Ezekiel Atoa Tamko, Hata Kama Wema Hataenda, yeye South Africa Ataenda Tu.


Aunty Ezekiel Atoa Tamko, Hata Kama Wema Hataenda, yeye South Africa Ataenda Tu.
Mwanadada Aunty Ezekiel amefunga mjadala uliokuwa ukiendelea baada ya kusemwa kwa maneno ya muda mrefu kuhusu uamuzi wa Diamond kuwataka yeye pamoja na Wema kwenda afrika ya kusini katika sherehe ya Tiffah.

Tamko la kwenda afrika ya kusini lilitolewa na Diamond mwenyewe na kusema kuwa katika watu kumi watakaokwenda ni lazima awepo Wema na Zari na ndipo Zari alipoanza kuwajibu katika mitandao kuwa hataki kuona watanzania watamchafulia nyumba.

Hata hivyo wengi walihisi kuwa tamko la Zari lingeweza kubadilisha mawazo ya wahusika lakini Aunty Ezekiel ameamua kujibu na kusema kuwa hata kama Wema hatokwenda Afrika ya kusini lakini yeye ataenda kwa sababu yeye ni  moja ya wanafamilia , lakini pia Zari pia ni wifi yake.

Ifike sehemu inabidi  tufunge mjadala maana kila siku ni aunt kuwa karibu na zari,wema na kama ni bethdei nitaenda tu.Hawa wote ni marafiki zangu kwa hiyo sasa siwezi kubagua eti kwa sababu wema aliachana na Diamond  wakati pia kule kwa Diamond kuna penzi wangu Iyobo  na isitoshe kwa upande mwingine Zari ni wifi yangu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad