Azam FC Watwaa Ubingwa na Kuifikia Rekodi ya Simba

Klabu ya soka ya Azam FC, imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Kombe la Kagame baada ya kuwafunga Simba mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliomalizika usiku huu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.


Wachezaji wa Azam FC na Simba kwenye moja ya matukio ya mchezo wa leo wa fainali ya Kombe la Kagame.

Mabao ya Azam FC katika mchezo wa leo yamefungwa na mshambuliaji Shaaban Idd pamoja na nahodha Aggrey Morris huku bao la Simba likifungwa na mshambuliaji Meddie Kagere.

Ushindi wa Azam FC unaifanya timu hiyo sasa kuifikia rekodi ya Simba ya kutetea ubingwa huo ambayo waliiweka mwaka 1992 wakitetea ubingwa waliouchukua mwaka 1992. Azam FC walitwaa ubingwa huu mwaka 2015 na wameutetea mwaka 2018 baada ya michuano hiyo kutofanyika katika miaka ya 2016 na 2017.

Aidha mshambuliaji wa timu hiyo Shaaban Idd ambaye ameshasajiliwa na timu ya Tenerife ya Hispania na atasafiri kwenda kujiunga nayo muda wowote kuanzia sasa, amefanikiwa kuibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao 8 katika mechi 5 kuanzia hatua ya makundi hadi leo fainali.

Azam FC sasa wametwaa kombe hilo kwa mara ya pili huku Simba ambao ndio mabingwa wa historia wa kombe hilo wakibaki na mara 6.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad