Baada ya Kuteuliwa na Rais Mbarawa Afanya Ziara Dawasco

Baada ya Kuteuliwa na Rais Mbarawa Afanya Ziara Dawasco
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof Makame Mbarawa amefanya ziara katika ofisi za DAWASCO ikiwa ni siku ya tatu baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo.

Prof Mbarawa amefika ofisini hapo na kufanya mazungumzo na wafanyakazi wa DAWASCO ambapo amesmshukuru Mungu na Rais JPM kwa kumpa nafasi hiyo.

“Namshukuru Mungu, pia namshukuru Rais kwa kunipa hii Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwani naamini nitakuja kuyabadilisha maisha ya Watanzania” -Prof Mbarawa

“Lazima tuwaletee maji Watanzania haiwezekani watu wapo hapa DSM na hawana maji, nataka mpate wateja laki nane na hamsini elfu, kwani itasaidia kuongeza mapato, tuhakikishe wateja wote wanaotaka maji wanapata maji”– Prof Mbarawa
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad