Baada ya Kutumbuliwa Mwigulu Akataa Kuongelea Mambo ya Siasa

Baada ya Kutumbuliwa Mwigulu Akataa Kuongelea Mambo ya Siasa
Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Dk Mwigulu Nchemba amesema masuala ya siasa atayazungumzia jimboni kwake.

“Mambo ya siasa siongelei, ukitaka kuongelea nifuate jimboni tuongelee maendeleo ya jimbo langu,” amesema Dk Nchemba.

Alisema hayo jana Julai 4, 2018 baada ya kumalizika mechi ya michuano ya Cecafa Kagame CUP katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kati ya Simba na Singida United.

Dk Nchemba alikataa kuzungumzia masuala ya kisiasa baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa Gazeti la Mwananchi.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad