Baada ya Msiba Mzito, Muna Aanza Kujirudisha Mitandaoni

MUIGIZAJI Muna Love ambaye hivi karibuni alipata msiba kwa kuondokewa na mtoto wake, Patrick, amefunguka na kusema kila binadamu hupitia magumu lakini haimanishi kwamba Mungu anakuwa amekuacha badala yake anakufanya uwe imara na kumwonyesha shetani kwamba ‘wewe ni mtoto wake’.

Muna ametoa kauli hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram na kumshukuru Mungu kwa yote aliyomtendea huku akisisitiza kwamba ataendelea kumtumikia muumba wake milele.

“Mungu anawapenda watu wote bila kujali wewe ni nani na unatabia gani mbele zake …na atatumia njia anazojua ili zikufikie na umtambue urudi kwake ukazaliwe upya… na hata pale anakupa jaribu sio kama hakupendi au anataka akuumize hapana, anakupa jaribu na pia anajua utaliweza na hatoweza kukuacha kamwe atakupa na njia za kupita.

“Mungu kwenye kila jaribu lile la aina yoyote jua yupo nyuma yako na anakukomaza ili kumuonyesha shetani kua wewe ni mtoto wake na anajivunia wewe sasa ,usiwaze kumuhukumu Mungu au kuumia kwanini umepitia hilo bali mshangilie na kumtukuza uone matunda atakayokupa 🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽

“Asikudanganye mtu Mungu awezi kukuacha upitie gumu bila kukupa njia na roho mtakatifu akakuongoza asante Mungu wangu nitakutumikia milele,” amesema Muna.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad